MAUAJI YA KUTISHA MWANZA WANAWAKE WATATU WAUAWA.. JESHI LA POLISI LATHIBITISHA

 

Na Samir Salum

Wanawake watatu ambao hawakufahamika Mara moja,wameuawa na watu wasijulikana na kisha miili yao kutupwa kandokando ya mto uliopo kwenye eneo la mtaa wa Mecco kusini,Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Miili ya marehemu hao iligunduliwa na Wapita njia,Jana January 19, 2022 majira ya saa sita  mchana ambao walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

VIDEO:MAUAJI YA KUTISHA MWANZA | WANAWAKE WATATU WAUAWA

kwa mujibu wa kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Gidion Msuya miili ya marehemu hao wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 30 imekutwa ikiwa na majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao yanayotokana na kukatwa na kitu chenye ncha kali.


kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Gidion Msuya Jeshi hill linafanya uchunguzi ili kubaini kiini cha tukio hilo.

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa ktk hospitali ya rufaa ya kanda Bugando jijini Mwanza.

VIDEO: MAUAJI YA KUTISHA MWANZA | WANAWAKE WATATU WAUAWA

Amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Jeshi hilo likiendelea na uchunguzi,na kuendelea kutoa taarifa kuhusu viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

MWISHO

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI👇

VIDEO: MAUAJI YA KUTISHA MWANZA | WANAWAKE WATATU WAUAWA


Post a Comment

Previous Post Next Post