Na Samir Salum
Wanawake watatu ambao hawakufahamika Mara moja,wameuawa na watu wasijulikana na kisha miili yao kutupwa kandokando ya mto uliopo kwenye eneo la mtaa wa Mecco kusini,Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Miili ya marehemu hao iligunduliwa na Wapita njia,Jana January 19, 2022 majira ya saa sita mchana ambao walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.
VIDEO:MAUAJI YA KUTISHA MWANZA | WANAWAKE WATATU WAUAWA
kwa mujibu wa kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Gidion
Msuya miili ya marehemu hao wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 30
imekutwa ikiwa na majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao yanayotokana
na kukatwa na kitu chenye ncha kali.
kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Gidion Msuya
Jeshi hill linafanya uchunguzi ili kubaini kiini cha tukio hilo.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa ktk hospitali ya rufaa ya
kanda Bugando jijini Mwanza.
VIDEO: MAUAJI YA KUTISHA MWANZA | WANAWAKE WATATU WAUAWA
Amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Jeshi hilo likiendelea na uchunguzi,na kuendelea kutoa taarifa kuhusu viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
MWISHO
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI👇
VIDEO: MAUAJI YA KUTISHA MWANZA | WANAWAKE WATATU WAUAWA
إرسال تعليق