TANZANIA YAPOKEA DOZI MILIONI 1.6 ZA CHANJO YA UVIKO-19 KUTOKA MAREKANI

 


TZUSAE

Tanzania imepokea  dozi milioni 1.6 ya chanjo dhidi ya UVIKO-19 aina ya Pfizer BioNTech zilizotolewa na Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Kimataifa wa Usambazaji chanjo wa COVAX.

Shehena hilo limepokelewa  leo Jumatano January 19, 2022 na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Rashid Mfaume kutoka kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Afya ya Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Ananthy Thambinayagam katika hafla fupi iliyofanyika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Hadi hivi sasa zaidi ya dozi milioni 4.5 za chanjo dhidi ya UVIKO 19 Zimetolewa na na Serikali ya Nchi ya Marekani Kwa ajili ya Nchi ya Tanzania.

 Shehena ya kwanza  iliyohusisha zaidi ya dozi milioni 1 za aina ya Johnson and Johnson ilipokelewa mwezi Julai 2021 na zaidi ya dozi milioni 3.5 za chanjo aina ya Pfizer BioNTech zilizoletwa kwa awamu tatu kati ya Novemba 2021 na Januari 2022.


Post a Comment

أحدث أقدم