Vikosi vya usalama nchini Sudan vimewauawa waandamanaji saba baada ya kuwafyatulia risasi wakati wa maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi.
Maandamano hayo yalitokea jana Jumatatu January 17,2022 kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum na kwenye miji mingine mikubwa ikiwa ikiwa ni wakati ambapo Marekani inajaribu kusaidia kuumaliza mzozo uliodumu kwa miezi kadhaa kwenye taifa hilo la Afrika Kaskazini.
Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa, Volker Perthes amelaani kile alichokiita ''matumizi ya risasi za moto kwa lengo la kuzuia maandamano'', akithibitisha kuwa takriban watu saba wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa, huku ubalozi wa Marekani mjini Khartoum ukikosoa mbinu za kuzuia ghasia zinazotumiwa na vikosi vya usalama vya Sudan.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Sudan kujizuia kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji. Wanachama tisa wa baraza hilo, ikiwemo Uingereza na Ufaransa wametoa wito huo, wakisisitiza kuhusu umuhimu wa kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza.
Vifo saba vilivyotokea jana Jumatatu vinaifanya idadi ya watu waliouawa katika maandamano kufikia 71 tangu jeshi lilipofanya mapinduzi Oktoba 25 yaliyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.
Chanzo DW KISWAHILI
إرسال تعليق