WAZIRI UMMY ASISITIZA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA ILI KUPUNGUZA KERO KWA WANANCHI



Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza juu ya kuboresha utoaji wa huduma za afya  ikiwemo katika huduma za mama na mtoto na huduma za lishe ili kupunguza kero na malalamiko kwa wananchi.

Ameyazungumza hayo leo katika kikao kati yake na  Viongozi wa Idara ya kinga kilichlfanyika mapema leo Januari 17, 2022 katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe. 


Katika kikao hicho wamefanya mapitio ya pamoja kuhusu mafanikio ,changamoto na vipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga nchini ili kupunguza maradhi,ulemavu na hivyo kupunguza gharama za matibabu na vifo miongoni mwa watanzania.

Mapitio yaliyofanywa kwenye kikao ni pamoja na ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ,huduma za chanjo,afya ya uzazi na mtoto,huduma za lishe,afya mazingira,Elimu ya Afya kwa Umma.


Aidha, wamejadili mikakati mbalimbali ya mapambano dhidi ya UVIKO-19, Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele(NTDs), Malaria,Kifua Kikuu na Ukoma na UKIMWI.

Maisho.

Post a Comment

أحدث أقدم