Vyanzo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa Mwanamke huyo mwenye ujauzito wa umri wa miezi mitatu alifika katika hospitali moja katika jiji la Peshawar akiwa amepigiliwa msumari wa sentimita 5 kichwani mwake na inadaiwa aliwafahamisha madaktari kwamba alitekeleza kitendo hicho yeye mwenyewe.
Baadaye, mama wa mabinti watatu alifichua kwamba mponyaji wa imani ndiye aliyehusika na kitendo hicho kiovu.
Daktari wa magonjwa ya mfumo wa neva Haider Suleman, ambaye alimtibu mwathiriwa katika Hospitali ya Lady Reading ingawa msumari ulikuwa umepenya kwenye fuvu la kichwa cha mwanamke huyo, haujafika kwenye ubongo wake.
Mume wa mwanamke huyo anadaiwa kutishia kumwacha iwapo angejifungua msichana wa nne.
Polisi wamethibitisha kuwa mamlaka imemtambua mwanamke huyo na mumewe.
"Afya ya akili ya mwanamke huyo haionekani kuwa shwari na anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. Mwathiriwa na mumewe wameamua kuchunguzwa na daktari wa magonjwa ya akili," polisi walisema.
Mumewe pia amejumuishwa katika uchunguzi.
Mkuu wa polisi wa Peshawar Abbas Ahsan amesema kuwa timu maalum imeundwa kumfikisha mwanamume huyo mahakamani ambaye alicheza na maisha ya mwanamke asiye na hatia.
Bw Ahsan aliongeza: "Timu hiyo pia itachunguza kwa nini tukio hilo halikuripotiwa kwa polisi na daktari anayetibu".
Kulingana na wahudumu wa hospitali hiyo, mwanamke huyo alikuwa akivuja damu na alipewa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa katika chumba cha upasuaji.
Dk Haider Suleman, daktari bingwa wa upasuaji wa neva, aliiambia Dawn, kwamba msumari ulikuwa umepenya ndani kabisa ya fuvu la kichwa cha mwanamke huyo na familia ilifanya majaribio ya kuutoa msumari huo nyumbani lakini ikashindikana.
"Alisema kwamba mwanamke katika eneo lake alifanya vivyo hivyo [kugonga msumari] na akajifungua mtoto wa kiume ingawa uchunguzi wa ultrasound ulionyesha mtoto wake ambaye alikuwa tumboni ni msichana," daktari alisema.
Wahudumu wa hospitali hiyo waliviambia vyanzo vya habari nchini humo kuwa mwanamke huyo alisema mumewe hakufurahishwa naye kwa sababu hangezaa mvulana, hivyo akatishia kumwacha.
Watoto wa kiume kwa kawaida hupendelewa kote katika nchi za Asia Kusini, ikiwa ni pamoja na Pakistan, kwa kuwa wanafikiriwa kuwapa wazazi usalama bora wa kijamii na kiuchumi.../
Endelea kufuatilia Mwanza Digital Habari Taarifa zaidi kukujia
إرسال تعليق