Na Samir Salum
Kampuni ya GSM imejiondoa kwenye udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mara baada ya makubaliano waliongia na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi kutozingatiwa.
Haya yametangazwa leo Jumatatu Februari 07,2022 kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa Biashara Mkuu wa Kampuni hiyo Allan Chonjo.
Amesema kuwa Kampuni hiyo imejitoa kudhamini ligi kuu Tanzania Bara ( NBC PREMIER LEAGUE ) leo Februari 07 chanzo kikidaiwa kuwa TFF na bodi ya ligi hawakutimiza Makubaliano ya Mkataba.

Aidha Allan amesema kuwa Ghalib Said Mohamed maarufu GSM ameamua kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti na Ujumbe wa Kamati ya Ushindi ya Timu ya Taifa Stars na kuwatakia Watanzania wote kila la kheri.
"Haya hayajawa maamuzi rahisi kwa kampuni ya GSM kwani tunatambua vipo baadhi ya klabu za mpira zitaumizwa pamoja na wadau mbalimbali na hatua hii haikuwa dhamira yetu kufikia uamuzi huu mgumu,” amesema Chonjo na kuongeza
"Tunaishukuru TFF, Bodi ya Ligi, Serikali, Waandishi wa Habari za Kimichezo na Wanahabari wote na tunawatakia kila kheri, GSM itaendelea kuacha milango wazi kwa Wadau wa Michezo katika kukuza Michezo yetu"
Nao Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF limethibitisha kupokea barua ya kuvunjwa kwa mkataba huo na limeeleza kuwa linafanyia kazi maamuzi hayo na kutoa taarifa kwa wadau wa soka.
Kuvunjwa kwa Mkataba huo baina ya Kampuni ya GSM na bodi ya ligi Kuu Tanzania Bara kumekuja ikiwa ni siku 76 tangu wasaini mkataba wa miaka miwili wa Shilingi bilioni 2.1 mnamo Novemba 23, 2021.
MWISHO
إرسال تعليق