RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo na upotevu wa mapato katika halmashauri hizo.
Rais Samia ametengua uteuzi huo leo Ijumaa Februari 04, 2022 akiwa njiani Magu jijini Mwanza akielekea Musoma mkoani Mara yanapofanyika maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
VIDEO: BREAKING NEWS: RAIS SAMIA ATUMBUA WAKURUGENZI WANNE
“Siku ile tunazitangaza fedha nilisema kama mkurugenzi anataka kuona rangi yangu halisi achezee hizo fedha, sasa kwa taarifa zilizopo, Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini, wakurugenzi wamechezea fedha. Mheshimiwa waziri (Waziri wa TAMISEMI) wakurugenzi hao nimewatengua sasa hivi” amesema Rais Samia
“Yule wa Geita endeleeni na uchunguzi, na mimi timu yangu iko pale inafanya uchunguzi naye wakiniletea na makossa kama haya nay eye attatenguliwa,” ameongeza Rais Samia.
Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa alisema kuwa Wizara hiyo ilipata taarifa za ubadhirifu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kuhusu Wilaya ya Buchosa na maeneo mengine.

Mwisho
إرسال تعليق