BREAKING NEWS: VIONGOZI WATANO WATENGULIWA ZANZIBAR

 




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ally Mwinyi ametengua uteuzi wa viongozi katika Wizara tatu ikiwemo Wizara ya elimu, Uchumi na Uwekezaji na wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

kupitia taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Februari 03, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said amesema kuwa Rais Dkt. Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Idara ta Utumishi na Uendeshaji katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, ndugu Omar Ali Omar na ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Tasisi ya Elimu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, ndugu Suleiman Yahaya.

Mhandisi Zena amesema kuwa Rais Dkt.Mwinyi ametengua uteuzi wa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Fatma Iddi Alli na ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Watoto katika Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na WatotoNasima Haji Choum.

Aidha Rais Mwinyi ametengua uteuzi wa Salum Ubwa Nassor, aliyekuwa Ofisa Mdhamini, Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Pemba.

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said amesema kuwa UTENGUZI WA NAFASI HIZO UNAANZA LEO.




Post a Comment

أحدث أقدم