Urusi imezuia matumizi ya mtandao wa Facebook unaomilikiwa na Kampuni ya Meta Platforms Inc's (FB.O) nchini kwao kile kilichoelezwa kupishana katika masharti ya vitu vya kuweka mitandaoni wakati huu wa vita yao na Ukraine.
Maamuzi hayo yameongeza presha kubwa kwa vyombo vya ndani ya Urusi ambavyo vinatishiwa kufungiwa ikiwa watatoa taarifa za uwongo kuhusu kinachoendelea kwa majeshi ya taifa hilo kuivamia Ukraine kama Urusi wanavyodai kuwa taarifa zinazopewa kipaumbele ni zile zinazowakandamiza wao.
Mkuu wa Kitengo cha Matukio ya Kimataifa wa Meta, Nick Clegg amesema: “Mamlaka za Urusi zilitutaka kuzuia taarifa zote zinazohusiana na vita katika mtandao wetu, tukawaambia hatuwezi kufanya hivyo, ndipo wakaamua kufungia huduma yetu.”
Source: Reuters
إرسال تعليق