Afisa wa zamani katika jopo la walinzi wa kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, Aisha Al-Fitouri, amedai kuwa kiongozi huyo bado yuko hai na kwamba aliyeuawa ni mmoja wa jamaa zake.
Al-Fitouri amesema katika mahojiano na runinga ya Russia Today kwamba, Gaddafi hakuingia mji wa Sirte, na kwamba mtu aliyeingia katika mji huo wakati wa mapigano ya ndani ya mwaka 2011 ni Hamid Bominyar Gaddafi aliyefanana naye sana. Amesema kiongozi huyo wa zamani wa Libya aliingia eneo la Bani Walid na kisha akaondoka zake.
TAZAMA VIDEO HAPA👇
VIDEO : AFISA USALAMA ATHIBITISHA GAADAFI KUWA HAI
Novemba mwaka jana, gazeti la Le Figaro la Ufaransa lilichapisha ushuhuda wa mwandishi wa habari Alfred de Montesquieu, ambaye aliingia katika chumba ambako mwili wa Gaddafi uliwekwa, siku moja baada ya kuuawa, na kusikiliza ushahidi wa watu walikuwapo wakati wa mauaji ya kiongozi huyo.
Mlinzi huyo Aisha al_fitouri Alipouluzwa kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilithibitisha kwamba aliyeuawa ni Muammar Gaddafi, baada ya kuchunguza vinasaba (DNA) vya mwili huo, alikana na kuhoji kuhusu umoja wa mataifa kutotoa uamuzi kuhusu kifo hicho na kutokabidhiwa mwili wake.

Montescu alisema kuwa "Katika chumba kile kikubwa ambako harufu kali ilikuwa ikifuka niliingia nikajikuta nipo mbele ya mwili wa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, kandokando ya maiti za mtoto na mlinzi wake mkuu."
Mlinzi huyo Aisha al_fitouri Alipouluzwa kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilithibitisha kwamba aliyeuawa ni Muammar Gaddafi, baada ya kuchunguza vinasaba (DNA) vya mwili huo, alikana na kuhoji kuhusu umoja wa mataifa kutotoa uamuzi kuhusu kifo hicho na kutokabidhiwa mwili wake.
"Hii sio kweli, Kwa nini Umoja wa Mataifa haujatoa uamuzi kuhusu suala hilo hadi sasa? na kwa nini mwili wake haujakabidhiwa?"- amesema
Libya ilitumbukia katika machafuko na vita vya ndani baada ya wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wale wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuishambulia nchi hiyo na kusaidia harakati za kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi Muammar Gaddafi hapo mwaka 2011.
Mwisho

إرسال تعليق