Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Jumamosi Februari 05,2022 Kamanda wa Polisi wa Rift Valley, Fred Ochieng amemtaja Mwanamke huyo Moleen Akinyi na kuwa Mwili wake umekutwa leo ukining'inia kwenye nyumba yake katika mji wa Gilgil Nchini Kenya.
Majirani Miili ya watoto iligunduliwa na majirani ambao waliita
Kamanda Ochieng amesema kuwa Moleen kabla ya kujiua kwa kujinyonga aliwaua watoto wake watatu, waliotambuliwa kama Brandon Pande mwenye umri wa Miaka 10, Trevor Pande mwenye umri wa miaka sita na Raddy Pande wa mwaka mmoja.
Ameeleza kuwa baada ya kukagua eneo la tukio walikuta barua aliyoiandika Moreen akielezea kutekeleza Mauaji hayo ambayo alimuandikia mumewe na kuongeza kuwa jeshi hilo linachunguza kubaini tukio hilo kama ni la mauaji ya kujitoa mhanga au limetekelezwa na mtu mwingine.
"Tutajua ikiwa ni mauaji ya kujiua. Inawezekana kwa mtu kuwaua na kupanga yote hayo. Tunachunguza,” amesema Kamanda Ochieng
Miili ya marehemu imehamishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali iliyopo katika Kaunti ya Nakuru.
Mwisho
إرسال تعليق