Mahakama katika mji wa Cologne nchini Ujerumani imemhukumu kifungo cha miaka 12 jela padri mmoja wa Kanisa Katoliki kwa makosa ya unyanyasaji kingono dhidi ya watoto.
Padri huyo mwenye umri wa miaka 70, pia ameagizwa kuwalipa walalamikaji watatu faini ya Euro elfu 50,000.
Hati ya mashitaka ilijumuisha jumla ya makosa 118 ya unyayasaji wa kingono uliofanyika kwa miaka mingi huku mwathirika mdogo zaidi akitajwa kuwa msichana wa miaka 9.
Waathirika wengine walijitokeza wakati wa kesi hiyo, ambapo mashtaka yaliongezwa na kusababisha mtuhumiwa kuwekwa rumande.
Hukumu hiyo inatolewa wakati wa uchunguzi mkali ukiendelea dhidi ya Kanisa Katoliki la Ujerumani baada ya ripoti huru ya hivi karibuni kubainisha miongo kadhaa ya madai ya unyanyasaji wa kijinsia na utovu wa nidhamu katika Dayosisi Kuu ya Munich.
📩Comment yako ni mhimu sana..
إرسال تعليق