Askari polisi saba wanaotuhumiwa kwa mauaji ya mfanyabiashara wa madini mjini Mtwara wamepandishwa kizimbani leo Jumanne katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara.Kesi ya tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Musa Hamis (25), mkazi wa Kijiji cha Ruponda Wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi, inayowakabili maofisa saba wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara ambapo watuhumiwa hao wamepandishwa kortini mara ya pili kwa ajili ya kutajwa kwa kesi hiyo.
Maofisa wanaotuhumiwa katika mauaji hayo ni Mrakibu wa Polisi, Gilbert Kalanje, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Mtwara (OC- CID), Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Charles Onyango na
aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara (OCS).
Wengine ni Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza, Mkuu wa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi John Msuya, Mganga Mkuu Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.
Januari 5, mwaka huu, watuhumiwa hao wanatajwa kula njama na kisha kumuua mfanyabiashara wa madini, Musa Hamis kisha kuutupa mwili wake katika Kijiji cha Hiari Wilaya ya Mtwara.
Inadaiwa kuwa Musa aliuawa wakati akidai fedha zaidi ya Shilingi milioni 33 zilizochukuliwa na maofisa hao baada ya kumkamata Oktoba 20, 2021 akiwa katika nyumba ya kulala wageni ya Sadina iliyoko mkoani Mtwara.
Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Januari 15, 2022 baada ya kukamatwa na kuhojiwa katika vituo mbalimbali vya polisi.
Kesi hiyo imetajwa leo na kuahirishwa hadi Februari 22, 2022 itakaposikilizwa tena.
Mwiaho
إرسال تعليق