Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Salum Hapi kuwasimamisha kazi Wakuu wa Idara za Fedha, Idara ya Mipango na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi wa baadhi ya Halmashauri za mkoa huo kufuatia ubadhirifu wa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo tarehe 06 Februari, 2022 wakati akihutubia wananchi wa Kwangwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Kwangwa, Wilaya ya Musoma Mjini mkoani Mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalim Julius Nyerere iliyopo eneo hilo.
Amewataka viongozi mkoani Mara kuacha ubinafsi na kufuja fedha zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo ya wananchi wa mkoa huo na badala yake wajikite katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Ameagiza Kamati zilizokuwa zikisimamia miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia fedha za Maendeleo ya ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 ziendelee kufuatilia ujenzi wa vituo vya afya na miradi ya Inuii inayotekelezwa nchini kote.
Amesema Serikali itatafuta fedha kwa Ajili ya kujenga vyuo vya ufundi stadi katika kila mkoa nchini ili kutoa fursa kwa vijana kuweza kujiajili wenyewe.
Awali Rais Samia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mara kuvunja mkataba na Mkandarasi anaejenga barabara ya Makutano hadi Sanzate Mkoani Mara.
amesema Mkandarasi huyo ameshindwa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 50 ambayo imeanza kujengwa tangu mwaka 2013 ambayo itagharimu shilingi bilioni 54.5 itakapokamilika pamoja na barabara ya Musoma -Makoja yenye urefu wa kilomita 5 ambayo ilianza kujengwa mwaka 2020 inayogharimu shilingi bilioni 8.2.
Aidha Rais Samia ameagua uongozi wa mkoa wa Mara kutafuta vvakandarasi wenye uwezo wa kifedha na mitambo katika kutekeleza miradi ya maendeleo mkoani humo.
Mwisho

إرسال تعليق