RAIS SAMIA AKARIBISHA WAFANYABIASHARA WA UFARANSA KUWEKEZA TANZANIA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Ufaransa kuwekeza Tanzania katika sekta za mifugo, kilimo, nishati, madini na maeneo mengıne yenye fursa.

Akilihutubia Shirikisho la Biashara la Ufaransa (MEDEF) mjini Paris, Rais Samia amefafanua kuııa Seıikali yake inachukua hatua muhimu kuweka mazingiıa muafaka ya kukuza sekta binafsİ.

Rais ameeleza kuwa Seıikali imefanya mabadiliko makubwa ya kisheria na kitaasisi kwenye sekta binafsi kuhakikisha kuna wepesi wa kuanzisha na kufanya biashara Nchini.


Pia, Rais Samia amesisitiza kuwa jitihada za Seıikali yake zimeendelea kuleta matokeo chanya, kama vile kituo cha uwekezaji kimesajili miradİ 256 mwaka 2021 kuzalisha ajira zaidi ya 53,00() na mtaji wa dola za kimarekani bilioni 3.7.

Wakati huo huo nchi hizo mbili zimetia saini hati ya makubaliano kati ya mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania na kampuni ya Kimataifa ya Bouygues Bâtiment (BBI) kwa ajili ya ukarabati wajengo la pili (Terminal II) la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.


Upande wa Tanzania katika hatua ya utiaji saini ulifanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Aliy Possi huku Ufaransa ukiwa umewakilishwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya (BBI), Bw. Eric Fleurisson.

Ufaransa inashika nafasi ya 35 kwa uwekezaji nchini Tanzania, ambapo tayaru kuna miradi 40 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 73.4, na kuzalisha ajira zaidi ya 1800 kufıkia sasa.

Post a Comment

أحدث أقدم