Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Ufaransa na baadae Ubelgiji kwa ajili ya ziara ya kikazi katika nchİ hizo.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zuhura Yunus leo Jumatano Februari 09,2022 amesema kuwa Rais Samia akiwa nchini Ufaransa anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.Rais Samia pia atashuhudia utiaji saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za miradi ya maendeleo, ushirikiano katika masuala ya uchumi wa buluu, usalama wa bahari, sekta ya usafiri na maendeleo endelevu.
Pamoja na masuala mengine, Rais Samia pia anatarajiwa kuzungumza na Watanzania waishio nchini Ufaransa.
إرسال تعليق