SOKO LA MBAGALA LATEKETEA KWA MOTO..DC JOKATE AUNDA KAMATI YA UCHUNGUZI



Soko la Mbagala rangi tatu lililopo Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam limeungua kwa moto usiku wa kuamkia leo Februari 13, 2022.

 Akizungumzia kuhusu tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo  amesema tayari wameunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha kuungua kwa Soko hilo.

Amesema kuwa kamati hiyo imepewa siku tatu hadi nne kuchunguza chanzo cha tukio hilo.

"Tumeunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha moto na tumeipa siku tatu hadi nne, kikubwa tumetoa maelekezo kwa Manispaa Kamati ya uchunguzi ikimalizika kazi Wafanyabiashara waruhusiwe kurudi Sokoni kufanya biashara huku ikiwekwa mipango ya kukarabati na kuboresha Soko hilo"

Kuungua kwa soko hilo kunazidi kuleta sintofahamu juu ya matukio ya masoko kuungua huku ikiwa imepita mwezi mmoja  tangu soko la Karume liungue mnamo Januari 15 huku chanzo cha moto kikiwa ni mshumaa. 

Endelea kufuatilia Mwanza Digital Habari Taarifa zaidi kukujia

TAZAMA PICHA HAPA CHINI





 

Post a Comment

Previous Post Next Post