Akizungumzia kuhusu tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema tayari wameunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha kuungua kwa Soko hilo.
Amesema kuwa kamati hiyo imepewa siku tatu hadi nne kuchunguza chanzo cha tukio hilo.
"Tumeunda Kamati ya kuchunguza chanzo cha moto na tumeipa siku tatu hadi nne, kikubwa tumetoa maelekezo kwa Manispaa Kamati ya uchunguzi ikimalizika kazi Wafanyabiashara waruhusiwe kurudi Sokoni kufanya biashara huku ikiwekwa mipango ya kukarabati na kuboresha Soko hilo"
Kuungua kwa soko hilo kunazidi kuleta sintofahamu juu ya matukio ya masoko kuungua huku ikiwa imepita mwezi mmoja tangu soko la Karume liungue mnamo Januari 15 huku chanzo cha moto kikiwa ni mshumaa.
Endelea kufuatilia Mwanza Digital Habari Taarifa zaidi kukujia
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
إرسال تعليق