TANESCO YATANGAZA TAREHE YA KUANZA KUTUMIA MITA ZISIZOHITAJI KUINGIZA TOKEN

 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kwamba kuanzia Julai mwaka huu litaanza kutumia ‘smart meters’ za umeme, ambapo mteja akinunua umeme utaingia moja kwa moja na umeme utawaka.


Maelezo hayo yametolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande akisema kwamba suala hilo limekuwa likiulizwa mara kwa mara lakini majibu yake yataanza kuonekana mwaka mpya wa fedha wa serikali.

“… ukinunua umeme, kama king’amuzi, pale pale kwenye simu yako unawaka, lakini hadi tuwe na smart meters ambazo zitaanza mwezi wa saba,” amesema Chande.

Jambo hili limekuwa kilio cha wananchi kwa muda mrefu wakitaka kuwepo mfumo ambao utawawezesha pindi wanaponunua umeme kwenye simu zao, wasilazimike kwenda kwenye mita zao kuingiza namba.

Hata hivyo, licha ya kuwa Chande hajaeleza, ‘smart meters’ ambazo zimeanza kutumika katika nchi nyingine zina uwezo wa kurekodi taarifa mbalimbali za mwenendo na utumiaji wa umeme, ili kumuwezesha mteja kuboresha matumizi yake.

Post a Comment

أحدث أقدم