Urusi imeshambulia miundombinu ya Ukraine kwa makombora, Ukraine inasema. Pia inasema imedungua ndege za Urusi - jambo ambalo Moscow inakanusha.
Misafara ya wanajeshi na vifaru imeingia Ukraine kutoka pande zote. Msafara mmoja umevuka kutoka Belarus kuelekea kaskazini mwa mji mkuu wa Kyiv. Mwingine umeingia kutoka Crimea kusini, ambayo Urusi ilitwaa kutoka Ukraine mnamo 2014
Takriban watu wanane wanaripotiwa kuuawa
Kuna foleni ndefu za magari huku wakazi wakijaribu kuukimbia mji mkuu wa Kyiv. Wakaazi wengine wametafuta makazi katika vituo vya treni. Waandishi wa BBC wanasema ingawa watu walitarajia shambulio hilo, ukubwa wa uvamizi huo umewashangaza
Ukraine imetangaza sheria ya kijeshi. Waziri wa mambo ya nje Dmytro Kuleba amehimiza vikwazo vikali, ikiwa ni pamoja na kuipiga marufuku Urusi kutoka kwa mfumo wa kimataifa wa uhamishaji pesa.
Bei ya mafuta imepanda hadi zaidi ya $100 kwa pipa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka saba. Sarafu ya Kirusi, imeshuka hadi chini kabisa dhidi ya dola na euro. Masoko ya Uingereza yameshuka
Misafara ya Magari wakiikimbia UkraineKumekuwa na matukio yakushutumu kutoka kwa viongozi wa dunia: Rais wa Marekani Joe Biden amesema vita hivyo vitaleta "kupoteza maisha kwa kiasi kikubw."Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema "amechukizwa"na "shambulio hilo lisilo na msingi wowote"
إرسال تعليق