NA SAMIR SALUM
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za Mauaji ya Dereva tax aliyeuawa kwa kunyongwa na kamba kisha kukatwa katwa na silaha zenye ncha kali wakina na lengo la kupora gari.
Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP amesema kuwa mauaji hayo yametekelezwa siku ya Jumatano Januari 26,2022 majira ya nne usiku ambapo Respikius Anastaz (55) dereva tax aliyekuwa akiendesha gari aina ya IST rangi nyeusi yenye namba T.143 DHV mkazi wa Isamilo Mkoani Mwanza aliuawa achanjo ikiwa ni kutaka kumpora wa gari.
amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ramadhan N'gazi amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Sylivester Renetus (30), Elizabeth Jackson (23), Robert Daud (42) mganga wa kienyeji na Ryabakamba Sekelwa (30) ambaye ni mke wa mganga wa kienyeji wote wakazi wa Kijiji cha Katunguru wilayani Sengerema.
Kamanda N'gazi amesema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano Januari 26,2022 majira ya nne usiku ambapo marehemu Respikius Anastaz ambaye ni Dereva tax alikodiwa na mtuhumiwa Sylivester Renatus akiwa na mkewe Elizabeth Jackson wakitaka kusafiri kutoka Mtaa wa Buzuruga Mkoani Mwanza kwenda wilayani Sengerema.
Ameeleza kuwa walipofika maeneo ya Kijiji Kasungamile, Wilayani Sengerema Mtuhumiwa Sylivester Renatus akiwa na mkewe Elizabeth walitekeleza mauaji hayo ambapo baada ya uchunguzi kufanyika iligundulika kuwa marehemu alishambuliwa kwa siraha zenye ncha kali katika maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo shingoni na mabegani.
"uchunguzi wa daktari umeonesha kuwa kabla ya kuchomwa kitu marehemu alinyongwa na kamba shingoni ili akose hewa na kisha kumshambulia kwa mapanga na visu katika mwili wake"-Kamanda Ngazi
Polisi wakiwa doria majira ya saa nne usiku walikuta gari hiyo na kuitilia mashaka ambapo waliisogelea na watuhumiwa walikimbia ambapo ufuatiliaji wa haraka ulifanyika na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa pamoja na mganga wa kienyeji.
"inadaiwa kuwa baada ya kufanya mauaji hayo walikwenda kwa mganga wa kienyeji ili wasafishwe aitwaye Ryabakamba Sekelwa ambaye amekamatwa pamoja na mumewe"-Kamanda Ngazi
Kamanda N'gazi amesema kuwa Tayari gari imepatikana ikiwa imefungwa namba bandia mbele na nyuma ambayo ni T 620 CGN na eno la tukio kumepatikana Visu viwili, panga moja, nyundo moja na simu mbili aina ya TECNO moja kubwa na nyingine ndogo na kamba moja.
Ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujiepusha na vitendo vya kihalifu kwani jeshi la polisi halitafumbia vitendo hivyo.
MWISHO
إرسال تعليق