WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO HAYA KWA TAKUKURU


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kutekeleza wajibu wa kuzuia vitendo vya rushwa kabla havijatokea katika jamii.

Waziri Jenista amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi  wa TAKUKURU akiwa kwenye ziara yake ya kwanza ya  kikazi kwenye taasisi hiyo, yenye lengo kujitambulisha  na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taaasisi hiyo.

Amesema kuwa gharama za kuzuia rushwa ni ndogo kuliko za kupambana na vitendo vya rushwa.

Mhagama amesema TAKUKURU ni kimbilio pekee la Watanzania wanyonge katika kuwaondolea tatizo la vitendo vya rushwa, dhuruma kwenye mirathi, hujuma zinazosababisha migogoro ya ardhi na ubadhirifu wa fedha za umma kwenye miradi ya kimkakati ambazo zinazotokana na kodi za wananchi.

“TAKUKURU ikitekeleza wajibu wake ipasavyo itaondoa vilio vya watu wengi ikiwemo wajane wanaodhurumiwa mirathi, Watanzania wanyonge wanaoingia kwenye migogoro ya ardhi kwa kudhurumiwa na wenye nacho, watoto wa kike wanaokabiliwa na changamoto ya vitendo vya rushwa mashuleni kutokana na jinsia yao ikiwa ni pamoja na kuondoa kilio cha watanzania na cha Mhe. Rais dhidi ya vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma zinazotolewa na Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo,” Mhe. Jenista amefafanua.


Majukumu yanayotekelezwa na taasisi hiyo ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu athari za rushwa, kuchunguza tuhuma za makosa ya rushwa, kuwafikisha watuhumiwa mbele ya vyombo vya sheria, na kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali ya mapambano dhidi ya rushwa.

Post a Comment

أحدث أقدم