Wakenya kuanzia leo Jumanne watalipia zaidi mafuta huku uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine ukiendelea kuathiri bei ya mafuta ghafi na bidhaa zake.
Mamlaka ya kudhibiti mafuta ya Kenya imesema bei ya petroli na dizeli itaongezeka kwa shilingi tano za Kenya sawa na ($0.044: £0.034)
Mamlaka hiyo aidha imesema bei ya mafuta ya taa, ambayo hutumiwa na watu wengi wa kipato cha chini Kenya kupika, "haitabadilishwa".
Mpango wa ruzuku ya mafuta ya petroli nchini Kenya umedumisha bei ya mafuta kwa miezi minne mfululizo.
Baada ya Urusi kuvamia Ukraine, mafuta ghafi ya Brent iliongezeka mara dufu katika kipindi cha miaka 14.
Bei ya bidhaa muhimu pia inatarajiwa kuongezeka nchini humo.
#ChanzoBBCSwahili
إرسال تعليق