MWANAFUNZI AFARIKI, KWA KUPIGWA RISASI SHULENI KISA KUZUIWA KUANGALIA MECHI YA MAN U..

Mwanafunzi amefariki kwa kupigwa risasi wakati polisi wakituliza vurugu za wanafunzi wa Shule ya Sekondari Gulu nchini Uganda, zilizotokana na kuzuiwa kutazama mchezo wa Man City dhidi ya Man United, Jumapili Machi 6, 2022.

Mwanafunzi huyo ametajwa kuwa ni Gabriel Rwotomiya ambaye alikuwa akisoma kidato cha tatu.

Shuhuda wa tukio hilo amesema marehemu alipigwa risasi hiyo akiwa kwenye mti wakati akijaribu kutoka katika vurugu zilizotokea. Baada ya hapo mwili wake ulichukuliwa na kupelekwa Gulu Regional Referral Hospital.

Wanafunzi wengine wamejeruhiwa wengi wao wakiwa ni wasichana. Baada ya tukio hilo wanafunzi 1,000 wamerejeshwa nyumbani kisha shule kufungwa kwa muda.

Kuzuiwa kushuhudia 'live' mchezo huo uliomalizika kwa Manchester City kushinda mabao 4-1 kulizidisha hasira za wanafunzi hao ambao walianzisha vurugu.

Baadhi ya mali na vitu kwenye shule hiyo vimeharibiwa ikiwemo katika maabara.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwonagweno ambapo ndipo shule hiyo ilipo, Alfred Otema amesema baada ya vurugu kuwa kubwa walinzi waliwasiliana na askari mbao walifika na kutumia bunduki kuzuia vurugu.

David Ongom Mudong ambaye ni Msemaji wa Polisi wa eneo hilo, hajatoa tamko kuhusu tukio hilo ambapo inadaiwa kuwa aliyefyatua risasi ni mmoja wa askari waliofika eneo la tukio.

Post a Comment

أحدث أقدم