UPELELEZI WAKAMILIKA, MTOTO ANAEDAIWA KUWALAWITI WENZAKE KUPANDISHWA KIZIMBANI...


Kesi nane za ukatili wa kingono kati ya 19 zinazohusu watoto waliodhalilishwa na mtoto mwenzao mwenye umri wa miaka 15 mkoani Iringa, zinatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki hii.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bulumbi amesema kuwa uchunguzi wa daktari umebaini kuwa watoto wote wamedhalilishwa na mtoto huyo ambaye anashikiliwa na polisi kulinda usalama wake.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwapatia zawadi za pipi, pesa na kuwaruhusu kuangalia televisheni nyumbani kwao, ili wakubali udhalilishaji huo.

Matukio ya ukatili wa kingono mkoani Iringa yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku, ambapo mwaka 2021 pekee watoto 384 walifanyiwa ukatili wa aina hiyo.

Wadau wa kupinga ukatili mkoani humo wamewataka wazazi kuchukua nafasi yao ya malezi ili kuwanusuru watoto na ukatili wa kingono.

Post a Comment

أحدث أقدم