WASIOAMINI KUWA KUNA MUNGU WATAKA KUPIGA MARUFUKU SIKU YA MAOMBI SHULENI

🇰🇪KENYA.

Chama cha wasioamini kuwa kuna Mungu nchini Kenya kimeiandikia barua wizara ya elimu kutaka kupigwa marufuku kwa siku za maombi katika shule za umma kabla ya mitihani ya kitaifa.

Kundi hilo linasema siku za maombi ni kinyume cha haki za wanafunzi.

Shule za umma zina utamaduni wa kuandaa siku za maombi kabla ya wanafunzi kufanya mitihani ya kitaifa.

Shule zimewaita wazazi wiki hii kujumuika katika utamaduni huo ili kuombea kipindi kizuri cha mitihani.

“Wakenya wengi wamepitia mfumo wa elimu ambapo uzingatiaji wa wa desturi za kidini ulikuwa wa lazima," chama cha wasioamini kuwa kuna Mungu kiliandika.

Kundi hilo linasema watoto wanapaswa kuachwa wafanye maamuzi yao wenyewe bila upendeleo kuhusu dini.

Sorce;BBC KENYA



Post a Comment

أحدث أقدم