Kenya Commercial Bank (KCB) Imezindua kiwanda Cha Kuzalisha Mafuta ya Kupikia kiitwacho GILITU INTERPRISES LTD kilichopo Mkoani Shinyanga.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo COSMAS KIMARIO alisema Kwasasa Benki ina mpango kabambe wa kushirikiana na wawekezaji wazawa kwa kuwapa mikopo ambayo inaweza kuwasaidia kuendeleza viwanda vyao ili wawe na uzalishajiwenye tija kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
Kimario alisema wamekiwezesha kiwanda cha Gilitu Interprises LTD Kwa kukipa mkopo ambao umekiwezesha kununua mitambo na vifaa vingine kwaajili ya uzalishaji wa mafuta ya kupikia (Alizeti) Ambapo mpaka sasa kiwanda hicho kimeanza uzalishaji na mafuta hayo yameanza kusambazwa kanda ya ziwa.
''Mikopo yetu imelenga sekta tofauti tofauti, mfano mkopo huu umelenga kwenye sekta ya wafanyabiashara wa viwanda ili kwenda sambamba na awamu ya tano wakati ule, uchumi wa viwanda, na awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan ikisema Kazi Iendelee''
Katika hali hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa GILITU INTERPRISES LTD Gilitu Nhila Makula Alisema kiwanda chake kinaenda kuongeza idadi ya wazalishaji wa Mafuta ya kula (Alizeti) ambapo itasaidia kuongeza upatikanaji wa mafuta hayo kwa wingi na hata kupunguza mfumuko wa bei kwenye mafuta hayo.
''Mafuta ya Alizeti ni Bora zaidi kwa afya kwaajili ya Mtumiaji, Hayana cholestro,'' Tuzidi tu kuwahimiza Watanzania wanunue mafuta ya ndani, yana ubora unaostahili, tuna wataalam ambao wanayazalisha kwa ubora, wanayasafisha kwa ubora, kwahiyo hiki kiwanda kitapunguza uhaba wa mafuta Tanzania.''
Makula pia aliwataka watanzania kuondoa dhana iliyojengeka kwao ambayo huwafanya wasijiamini kama wanaweza kufanya mambo makubwa katika uwekezaji wa viwanda hali inayosababisha kuona kuwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi ndio zenye ubora kuliko zinazozalishwa na Wazawa.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa kiwanda Cha GILITU INTERPRISES LTD - Shinyanga
إرسال تعليق