CLUB ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza {MPC} imesema Katika uongozi wa Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan, kumekuwepo na uimalikaji wa hali ya juu wa uhuru wa vyombo vya Habari Nchini.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa CLUB Hiyo Edwin Soko alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ua Uhuru wa Vyombo vya Habari ambako kwa mkoa wa Mwanza, Maadhimisho hayo yameadhimishwa na Kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel.
Soko Alisema chini ua Uongozi wa Rais Samia, Takribani Magazeti Manne yaliyokuwa yamefungiwa ya Tanzania Daima, Mawio, Mseto, Blogu moja na Mwanahalisi yalifunguliwa kutoka kifungoni.
''Marekebisho ya Sheria ya Posta na Mawasiliano ya 2010 na kanuni zake zikiwemo kanuni za maudhui mtandaoni na kanuni za maudhui ya utangazaji na kuwepo kwa utayari wa mapitio ya Sheria ya haki ya kupata Taarifa ya 2016 ni mambo aliyoyafanya katika kipindi hiki'' alisema Soko.
Soko Alifafanua kuwa utayari wa serikali ya awamu ya sita ya kukutana na wadau na kufanya majadiliano chini ya waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye hatua hiyo zinaleta matumaini kiasi ya Tanzania Kuheshimu Uhuru wa Vyombo vya habari tofauti na miaka mitano iliyopita {2015-2020}, ambapo uhuru wa vyombo vya habari uliporomoka na kuifanya Tanzania Kushika nafasi ya 53 duniani ya kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari.
Alisema licha ya vyombo vya Habari kuwa na mchango mkubwa hasa wakati huu wa uchumi wa kidigitali wa kuhabarisha Umma kupitia mawimbi na kusisitiza kuwa vyombo vya habari vya Mkoa wa Mwanza ambavyo ni wanachama wa MPC vitaendelea kufanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Mkoa na Serikali kuu kwa manufaa mapana ya Taifa.
Akifungua Rasmi maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel ambaye alichangia chama kiasi cha sh. milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi yake, alisema serikali yake itaendelea kufanya kazi kwa karibu na vyombo vya habari vya Mkoa wa Mwanza. ''Hamhitaji kuweka appointment kuja ofisini kwangu, mkiwa na jambo linalohusu Mkoa wetu njooni pale ni nyumbani kwenu, huhitaji kwenda nyumbani ukamuomba mzazi ruhusa,'' Alisema.
Alisema Waandishi wa Habari nchini wana nafasi kubwa katika kulinda umoja wa kitaifa na maslahi ya nchi endapo watatumia taaluma na kalamu zao kwa ufanisi.
إرسال تعليق