Na Paul Nenetwa - MWANZA
NBC Wamejipambanua zaidi katika kuboresha huduma kwa wateja wao ili kuwapa nafasi ya kukuza mitaji yao kupitia huduma mbalimbali zitolewazo na Bank hiyo ikiwemo account rafiki zisizokuwa na makato kwa wateja pamoja na mikopo yenye Riba nafuu kwa Wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine Bank ya NBC Kwa kuwajali wajasiriamali wadogo wadogo ilitambulisha huduma mpya kwa wageni waalikwa wakiwemo wafanyabiashara pamoja na wadau wengine wa Bank Hiyo Ili kuwafanya wachangamkie fursa zilizopo ndani ya Bank hiyo.
Mkuu wa kitengo cha wajasiriamali wa Benki ya NBC Mussa Mwinyidaho Akizungumza na wageni waalikwa ambao ni wafanyabiashara wadogo na wakubwa katika Hafra iliyoandaliwa kwaajili kujadili fursa mpya zinazopatikana ndani ya Benki Hiyo.
Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Aliipongeza NBC kwa kujipambanua kwa wateja hasa kuwapa Fursa wajasiriamali wadogo wadogo ili waweze kuukuza uchumi wao na hata uchumi wa Taifa kwaujumla kupitia Kodi wanazolipa kutokana na Biashara zao.Eng. Gabriel Alisema, Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji ambao watachangiza katika ongezeko la kukuza uchumi wa wananchi hasa wakazi wa jiji la Mwanza.
Mwisho.
إرسال تعليق