OJADACT YAJA NA MAPENDEKEZO MGOGORO UNAOENDELEA LOLIONDO MKOANI ARUSHA.

 Na Paul Nenetwa - Mwanza.



Chama Cha Waandishi wa Habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) Kikiongozwa na Mwenyekiti wake Edwin Soko,  Kinalaani matukio ya kihalifu yanayoendelea kwenye zoezi la uwekaji mipaka ya eneo la Loliondo, Mkoani Arusha.



Matukio ya Vurugu yanayoripotiwa kupitia kauli za viongozi ikiwemo ile ya Waziri Mkuu Aliyoitoa Bungeni, Kauli Iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella na ile ya Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa Pamoja na Taarifa zinazozagaa Kupitia Mitandao ya Kijamii, ni wazi kuwa kumekuwa na uhalifu wa kisheria unaovunja haki za binadamu kwa kiasi kikubwa.






Taarifa ya kifo cha Askari wa Jeshi la Polisi Garlus Mwita (36) na Taarifa nyingine za matumizi ya nguvu yanayoathiri utulivu na zoezi la uwekaji mipaka na utulivu wa wananchi wa Loliondo Yanaswa kukomesha mara moja.


Katika Hatua hiyo OJADACT inatoa mapendekezo Yafuatayo,

  -mapendekezo kwa serikali

.Itekeleze zoezi la uwekaji alama za mipaka kwa utulivu na ushirikishi baina yeke na viongozi wa kaya za Loliondo.

.Isikilize hoja zinazotolewa kupitia kamati shirikishi za utatuzi wa mgogoro wa Loliondo

.Ihakikishe ina wajibu wa kulinda amani na utulivu wa eneo la Loliondo

       -Mapendekezo kwa wakazi wa Loliondo

.Waepuke matumizi ya nguvu na silaha za jadi dhidi ya maafisa wanaoshiriki zoezi la uwekaji alama za mipaka.

.Watumie njia shirikishi kuwasilisha hoja muhimu walizonazo juu ya utekelezwaji wa zoezi la uwekaji alama za mipaka Loliondo.

     -Ushauri kwa jamii

.Iepuke kusambaza taarifa zinazoweza kukuza mgogoro wa Loliondo na kuleta Taharuki.

      -Mapendekezo kwa vyombo vya habari 

.Vitumie weledi wa kitaaluma kwenye kuandika habari za mgogoro huu ili kuaksi uhalisia unaoendelea.

.Viwe makini kwenye kuchagua vyanzo vya taarifa vya mgogoro huu pamoja na matumizi ya picha halisi za mgogoro.

.Vitumie Uandishi wa kuleta suluhu (Solution Journalism) kwenye kuandika habari za mgogoro huu.

.Vitoe haki sawa kwenye kuweka mizania ya habari zinazohusu Loliondo 

.Vijue vina haki ya kuandika habari za Loliondo kwa kujisimamia bila kuingiliwa kimaudhui.

       -Mapendekezo kwa jeshi la polisi   

.Lihakikishe linachukua hatua za kuwatafuta na kuwakamata wale wote waliohusika kwenye matukio ya mauaji.

.Lihakikishe linatoa ulinzi wa raia na mali zake kama sheria ya uanzishaji wa jeshi la polisi inavyoelekeza.

.Lihakikishe linatoa taarifa za mara kwa mara za watuhumiwa linaowashikilia.





Post a Comment

أحدث أقدم