AICT TANZANIA WAADHIMISHA MIAKA 80 YA UMISHONARI {AFRICA INLAND MISSIONARY}

 


     Kanisa la AICT Tanzania Limeadhimisha miaka 80 ya utumishi wa umishionari {African Inland Mishionary}  maadhimisho hayo yamefanyika katika kanisa la Pastoreti ya Butundwe na kanisa la pamoja la Nyasembe.



Maadhimisho hayo yameongozwa na Askofu wa kanisa la AICT Tanzania Mussa Masanja Mwagwesela, Maaskofu, Wachungaji, Wainjilisti, Viongozi wa Kiserikali, Kwaya mbalimbali, waumini wa kanisa na wakristo wengine kutoka maeneo mbalimbali.


      Mwakilishi wa African Inland Missionary Mchungaji Andrew Andersen amesema kipindi huduma ya Umisionari inaanza, lengo lilikuwa ni kusaidia kujenga makanisa na kusukuma maendeleo ya maeneo husika ambayo makanisa hayo yalianzishwa.


     Akizungumza Kuhusiana na Umisionari wa eneo la Nyasembe Butundwe, Askofu Mkuu wa AICT Tanzania Mwagwesela amesema maadhimisho hayo yamebeba Maudhui ya kuendeleza kile ambacho kilianzishwa na kuboreshwa kipindi cha nyuma.


       Nae Mbunge wa Jimbo wa Jimbo la Busanda Mhandisi Tumaini Magesa Amesema wao kama wawakilishi wa wananchi wanashukuru yote yaliyofanywa na wamishionari hao wa AIM {African Inland Misionary}

Aidha kwa niaba ya Maaskofu, Wachungaji na Wainjilisti Walioshiriki katika Maadhimisho hayo wamesema wamefurahishwa na kile walichokifanya wamishionari wa AIM na Kuomba Waendelee kusaidia maendeleo nchini Tanzania.

 
 

Post a Comment

أحدث أقدم