MWENGE WA UHURU WAZINDUA TAWI JIPYA LA BENKI YA CRDB BUHONGWA JIJINI MWANZA

 


Na Paul Nenetwa - Mwanza

Mwenge wa uhuru umezindua Tawi la Benki ya CRDB lililopo kata ya Buhongwa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Ambapo tawi hilo litakwenda kusogeza huduma kwa wateja wake wanaoishi kata buhongwa na maeneo jirani na kata hiyo.

     Akizungumza na wakazi wa eneo la buhongwa waliojitokeza katika uzinduzi Wa tawi la benki hiyo Pamoja na kuushuhudia mwenge wa uhuru ambao umekimbizwa maeneo tofauti ya wilaya hiyo, Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahili Geraruma Amesema kwa sasa wananchi wa kata ya buhongwa na maeneo ya jirani wamesogezewa huduma za kifedha na benki hiyo hivyo kuwataka    watumie fursa ikiwemo kufungua akaunti kupitia benki ya CRDB.

    kwa upande wake meneja wa benki hiyo kanda ya ziwa Lusingi Sitta amesema benki hiyo imeboresha huduma zake ikiwa ni pamoja kuongeza matawi yake nchini kutoka matawi 19 miaka ya nyuma hadi kufikia matawi 168 kwa sasa ambayo yako nchi nzima

   Katika hatua nyingine Amesema wamepanua wigo wa katika huduma zao kwani kwa sasa asilimia kubwa inayonufaika na benki hiyo ni kundi la wafanyabiashara wadogo wadogo pamoja na wa kati kwa kupata mikopo yenye masharti na riba nafuu hivyo kuwawezesha kukuza mitaji yao ikiwemo kuongeza kipato chao na hata kipato cha Taifa kupitia kodi wanazolipa.



Post a Comment

أحدث أقدم