WATENDAJI WA SERIKALI WATAKAOTUMIA TAKWIMU ZA WANANCHI KINYUME NA UTARATIBU KWENYE ZOEZI LA SENSA KUKIONA CHA MOTO.


Na Paul Nenetwa.  Magu-Mwanza.

Watendaji wa serikali watakaozitumia Takwimu za wananchi ambazo zitakusanywa kwenye Zoezi la Sensa ya watu na makazi August 23 2022 kinyume na Utaratibu watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Hayo Yamesemwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Sahili Gerarumo wakati wa mbio zamwenge wilayani Magu ambapo amesema Taarifa Zitakazotolewa na wananchinkwenye zoezi hilo Zinatakiwa kuwa siri baina ya mwananchi na serikali na zitatumika kwaajili ya zoezi la sensa pekee na si vinginevyo hivyo aliwataka Watendaji mbalimbali wa Serikali kutojaribu kuzitumia Taarifa hizo kwenye matumizi mengine Tofauti na zoezi la sensa peke yake.

 ''Taarifa za wananchi zitatumika kwa madhumuni ya sensa tu na si vinginevyo, kwahiyo ndugu zangu msiwe na wasi wasi wakati wa kutoa taarifa zenu, Viongozi mtakaohusika kwenye zoezi hili hakikisheni mnakuwa waadilifu, mnakuwa wema, msitoe taarifa hizo ndivyo sivyo''


katika hatua nyingine mwenge wa uhuru umekimbia zaidi ya kilomita 120 na kuifikia miradi sita {6} ndani ya wilaya ya Magu yenye jumla ya shilingi Bilioni moja na milioni 23, ambapo baadhi ya miradi imewekewa mawe ya msingi, huku mingine ikikaguliwa na mingine kuzinduliwa na mwenge huo ndani ya wilaya hiyo.


Nae mkuu wa wilaya ya magu Salumu Kali Alitumia mbio hizo za Mwenge wa uhuru kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika mwezi Agust mwaka 2022 nchi nzima huku Akiwataka wananchikujiandaa kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hilo.



Post a Comment

أحدث أقدم