CRDB BANK SUPER CUP YAACHA GUMZO JIJINI MWANZA, YAMWAGA PESA KWA WATUMISHI WAKE KUPITIA MICHEZO

 

Benki ya CRDB Imehitimisha mashindano yake ya CRDB BANK SUPER CUP 2022 katika michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete huku washindi wakijizolea zawadi mbalimbali zikiwemo medali, vikombe pamoja na pesa Taslimu.

    CRDB ilianzisha Mashindano haya ikiwa na lengo la kuwekeza katika Afya kwa watumishi wake kwa kuhakikisha wanatambua thamani ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuepukana na magongjwa nyemelezi yanayoweza kuepukika kwa kufanya mazoezi.


      CRDB SUPER CUP 2022 Imehitimishwa katika uwanja wa CCM kirumba Jijini Mwanza kwa michezo mikubwa mitatu, ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa ni mchezo wa kumpata mshindi wa tatu katika mpira wa miguu, huku ikifatiwa na michezo miwili ambayo ilianza kwa wakati mmoja, ambayo ni michezo ya fainali katika mpira wa miguu na fainali katika mpira wa pete.


Aidha mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB Ndg.Abdulmajid Nsekela amesema michezo hiyo inawaweka pamoja kama watumishi na kuwapa hamasa ya kufanya kazi.

    ''michezo hii inatuweka pamoja na kwa kufanya hivi wafanyakazi wetu wanakuwa na hamasa ya kufanya kazi na kuwa wabunifu, lakini kubwa ni kuhakikisha wafanyakazi wetu wanakuwa na Afya njema kupitia michezo hii'' amesema  Nsekela.



kwa upande wa washiriki wa mashindano hayo ambao wote ni wafanyakazi kutoka benki ya CRDB wameishukuru benki hiyo kwa kuandaa utaratibu wa kuwakutanisha pamoja wafanyakazi wote ili kufahamiana, kuhamasishana kuhusu umuhimu wa kulinda afya zao hasa kwa kufanya mazoezi huku wakiuomba uongozi kuendelea kuboresha mashindano hayo ili yawe bora zaidi.



Post a Comment

أحدث أقدم