kampuni ya kubashiri ya betpawa imegawa vifaa vya michezo kwa timu nne mkoani Mwanza ikiwa ni mpango endelevu wa kurudisha kwa wanamichezo faida wanayoipata.
Vifaa hivyo vimetolewa katika viwanja vya bwiru press ambapo yamefanyika mashindano madogo kuelekea fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo inategemea kuchezwa june 1 2024 katika viwanja vya wembley huko London, mchezo utakaowakutanisha Borussia Dortmund dhidi ya Real Madrid.
"Tunajua kuna tukio kubwa Sana la mashindano ya UEFA kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund, na sisi kama petpawa mara nyingi huwa tunakuja kushiriki na wanamichezo, Kufurahia na kutoa zawadi mbalimbali,
" Kwahiyo tumekuja leo kutoa jezi na mipira kwaajili ya kuwahamasisha vijana kupambania ndoto zao kuwa wachezaji wakubwa'' alisema Bora ndanyungu meneja masoko wa petpawa afrika mashariki.
Hata hivyo malengo ya betpawa ni kuendelea kusaidia ukuaji wa sekta michezo kwa kutoa vifaa mbalimbali vya michezo nchini ambapo mpango huo umeanzia jijiji Dar es salaam, dodoma na hatimaye jiji la mwanza kabla ya kuelekea mikoa katika mikoa mingine.
إرسال تعليق