ZAIDI YA WANAFUNZI 3000 KUNUFAIKA NA MIUNDOMBINU YA UFUNDISHAJI ELIMU YA TEHAMA WILAYA YA ILEMELA.

 

Zaidi ya wanafunzi elfu tatu (3000) wa shule ya msingi mnarani na bwiru pamoja na shule ya sekondari mnarani na kitangiri zikiwemo shule kongwe za bweni bwiru wasichana na bwiru wavulana wataanza kunufaika na miundombinu wezeshi itakayowasaidia kujifunza elimu ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).


Hali hiyo inakuja mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa BITEC (bwiru information technology education centre) uliojengwa na SOGEA SATOM (ISSA) ambao utawasaidia wanafunzi kujibu maswali ya utahini katika mahiri za TEHAMA.

Mradi huo umekamilika kwa gharama ya Shillingi milioni 102, 595 , 800 huku ukiwa na vifaa vya kujifunzia kama kompyuta mpakato (laptop) 35, zenye thamani ya sh. Milioni 24, pamoja na samani za meza ambapo vyote viko tayari kwa matumizi.

Manufaa ya mradi huu ni makubwa kwakuwa umekuja wakati kuna mifumo mingi ya utendaji kazi ikiwemo FFARS, PEPMIS, PREM, BEMIS, NEST n.k ambayo inahitaji kuwa na mtandao wa internet kuweza kuitumia.

Hata hivyo umuhimu wa mradi huu utaonekana zaidi kutokana na uwepo wa Tahasusi mpya ya PMCS (physics, mathematics and computer science) katika shule za bwiru wasichana (bwiru girls) na Bwiru wavulana (bwiru boys) ambapo wanafunzi wa mchepuo huu kituo chao kikuu cha mafunzo kitakuwa ni hapa BITEC.

Mradi huo umezinduliwa na katibu tawala wa wilaya ya ilemela adv. Mariam Msengi kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo mwalimu Hassan Masala ambapo amesema utaenda kusaidia kuongeza uelewa kwa wanafunzi wa shule hizo kuhusu masomo ya TEHAMA.

Aidha amewataka walimu wakuu na wakuu wa shule zote zitakazonufaika na mradi huo kuhakikisha wanaitunza na kuilinda miundombinu hiyo ili itumike na vizazi vinavyokuja.


Mradi huo umetekelezwa kwa fedha za wafadhili kwa asilimia 100 mpaka kukamilika kwake ambapo ujenzi wa mradi huo ulianza Disemba 5 mwaka 2023 na umekamilika mwezi juni mwaka 2024.

Post a Comment

أحدث أقدم