MWANAHARAKATI wa masuala ya kijamii na Mwanamziki maarufu Tanzania . Agness Suleiman Kahamba amekabidhiwa tuzo yake kupitia taasisi yake ya TUPAZE SAUTI FOUNDATION baada ya kutangazwa mshindi kipengele cha ‘Notable in community Development’ katika tuzo za ‘100 Most Notable Africans Awards’ zilizofanyika nchini Rwanda.
Binti huyu wa kitanzania alijipatia umaarufu barani afrika na duniani kote na kusababisha kupata tuzo kadhaa kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ndani ya muda mfupi katika kutetea haki za wanawake, vijana na watoto.
Tangu mwaka 2018, Agness ambaye ni Mwasisi na Rais wa Tupaze Sauti Foundation (TSF), taasisi isiyo ya kiserikali (NGO) na Balozi wa Kutetea Unyanyasaji dhidi ya Watoto, ameshatwaa tuzo kadhaa ambazo zimemfanya kuwa miongoni mwa Watanzania waliopata umaarufu katika medani ya kimataifa.
Kupata kwa tuzo hii ya wanawake maarufu Afrika imemfanya Agness kuwa miongoni mwa wanawake 100 mashuhuri katika masuala ya familia na maendeleo ya jamii.
Tuzo hii imekuja baada ya mwaka jana kupata tuzo ya mmoja ya watu 100 wa juu waanzilishi wa NGO. Alipata tuzo hiyo kwa kutetea na kuleta mabadiliko katika maisha ya watu kwenye masuala ya usawa wa jinsia, ukatili dhidi ya watoto, elimu, afya, uwezeshaji wanawake, haki za binadamu na maendeleo ya jamii.
Tuzo hizo zilikuwa mwendelezo wa ile aliyoipata mwaka 2018 baada ya kushika nafasi ya 16 ya Tuzo ya Vijana 50 wa Tanzania wenye Ushawishi zaidi katika masuala ya kijamii.
“Malengo ya asasi yetu ni pamoja na elimu kwa jamii, kuwawezesha vijana kujitambua, ujasiriamali kwa wanawake na kutambua haki zao. Pia uhamasishaji katika kukabilinana na matukio ya dharura yakiwemo magonjwa ya mlipuko kama ilivyokuwa UVIKO- 19,” alisema agness.
“Mimi ni mwanamke, mama, binti na kijana, hivyo niliona hayo maeneo ni ya muhimu kuyafanyia kazi kwa sababu ya- nanihusu kwa namna tofauti. Makundi haya ndiyo yenye shida katika jamii. Kwa serikali pekee ni vigumu kutatua shida za makundi hayo bila msaada wa wadau. Kwa hiyo niliona ni fursa kuanzisha asasi hii kuwezesha jamii kupaza sauti.
Agness alibainisha kwamba wanawake katika baadhi ya maeneo, hasa vijijini ambako mwamko wa elimu kwa mtoto wa kike ulichelewa, kumekuwa na dhana iliyojengeka kutokana na imani kwamba mwanamke anapoolewa hawezi kuachana na mume hadi kifo kitakapowatenganisha.
Hali hiyo, anasema imewafanya baadhi ya wanawake kuamini kuwa ni mwiko au dhambi kuachana na mume baada ya kufunga ndoa. Alisema kutoka- na na fikra hiyo, baadhi wanaogopa aibu ya kuonekana kuwa wameondoka kwa waume zao, hivyo wanalazimika kuvumilia hata wakipata vipigo, ulemavu wa kudumu hata kupoteza viungo.
إرسال تعليق