WADAU WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA NEST ILI KUHAKIKISHA THAMANI YA FEDHA KATIKA UNUNUZI.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Mhandisi Chagu Ng'homa amewataka wadau wa ununuzi nchini kutumia Mfumo wa Kielekitroniki ipasavyo ili kusaidia kupata wazabuni wenye gharama zinazolingana na thamani ya fedha zinazolipwa.

Ametoa wito huo leo tarehe 20 januari, 2025 kwa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati akifungua mafunzo yaliyofanyika Rock City Mall- Mwanza ya mfumo wa Usimamizi na Ununuzi wa Umma Kielektroniki uliowakufanisha washiriki kutoka taasisi mbalimbali nchini.

Amesema, washiriki wanapaswa kuwa wazalendo kwenye kazi zao kwa kuzingatia kuwa wanatakiwa kulinda rasilimali fedha za nchi wakati wa ununuzi kwa kuwashindanisha wazabuni kwa mujibu wa sheria.

"Mfumo huu umeletwa mahsusi ili kusaidia kuongeza wigo wa ushiriki wa wazabuni, kukidhi mahitaji na matarajio ya watumiaji pamoja na kurahisisha mchakato wabuombaji zabuni hivyo nendeni mkazingatie hayo ili kulisaidia taifa." Chagu.

Aidha, ametoa wito kwa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) kuendelea kuboresha mfumo huo ikiwa ni katika kuweka mazingira rafiki kwa wazabuni na kutoa mafunzo kwa taasisi nunuzi ili kufikia malengo yalivyokusudiwa.

Vilevile, ametoa pongezi kwa mamlaka hiyo kwa jinsi wanavyoendelea kuboresha mfumo huo ambao Mhe. Rais mwenyewe aliuzindua mahususi kwa ajili ya wadau kufuatilia mchakato kwa uwazo na kuona thamani ya fedha.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Robert Kalunde amesema wameandaa mafunzo hayo ya siku 5 yanayowakutanisha washiriki zaidi ya 230 kutoka Taasisi mbalimbali nchini ili waujue vizuri mfumo huo na kufikia malengo kwenye ununuzi.



Post a Comment

أحدث أقدم